Nikianza kuongea juu
ya campus wasee hunicheka, wengine husema
ni hali ya kujidai au hata kujipenda, but Campus life jo imenijenga, two years
down the line jo na siezi teta, mazuri jo maishani yameni teka, kaa maji sa
nafuata mkondo, namfuata yesu niite mwana kondoo, mienendo yangu ka nile sa hayana kikomo, fikira safi ni ka
imeoshwa na omo, brotherhood nimeget campo naipenda no homo, na luv nimeget kwa
msupa haina kikomo. Intellectual advancement ndio main agenda, but msupa wa me siwezi
kosa mpenda, kukata maji matym me hupenda but kulala Kwa mtaro thanks god
sijawai tenda. Tangu niingie campo life imekuwa na drama, inaniwai utadhani
nimekuwa drum nayo imekuwa drammer, nasema ukweli na sitazingatia grammer, juu
nisipoeleza kile itafuatilia ni gharama.
Sa nikiongelea kile nimeona, najua nitawagusia wengine
hasira watanoa, but atleast nitakuwa nimesave wengine ka Noah, wengine
watanitake for a ride ka Toyota noah.
Dame ame join campo young and innocent, back kwa village ye ni kioo cha
jamii, fika campus anatoa ignorance, semester ya kwanza ashakuwa simu ya jamii.
Boy naye ashajifanya babayao, madem kuwa play anawabadilisha ka chupi, hawa wasee maisha yao
sa fupi, future wameiruin juu ya vitendo vya kimaudhi
Si kila kitu about campus jo ni mbaya, dame ametoka kwao
mashamba ka hajui fashion, urembo nayo anayo kwa wengine ishakuwa tisho, vipodozi ashajipaka stage ashajipata,
ku cat walk miss university ashaipata. Ku traverse the country aki represent
uni yake.
Watu husema wamepitia school of life, but hio life ni
incomplete ka hujapitia campus life, ma drama hukuandama za education, za
religion za mapenzi na ukahaba usi forget
za siasa, though kile ina boo campus life ni short ka kinyasa, na bila
mpango huku nyanyasa, but still yet me napenda campus life, na siwezi I 4get
hadi nirudi six feet under.